Pamoja na magongo mikononi huku akiwa anachechemea lakini hiyo haikumzuia mlinda mlango wa Bayern Munich Manuel Neuer kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi sana bibie Nina Weiss.
Neuer alionekana kanisani akiwa ndani ya suti yake nyeusi huku akitembea kwa magongo ambapo kushoto kwake alikuwepo mrembo huyo mwwemye umri wa miaka 23 katika harusi iliyofanyika nchini Italia.
Neuer mwenye miaka 31 alikuwa mpenzi wake huyo walikuwa wapenzi tangu mwanzoni mwa michuano ya Euro mwaka jana na wawili hao kwa muda mrefu walikuwa na ndoto ya kuoana ambayo imetimia jana.
Wakati Neuer akifunga ndoa na mpenzi wakehuyo, wenzake wa timu ya taifa walikuwa uwanjani kuikaribisha timu ya taifa ya San Marino katika mchezo ambao timu ya taifa ya Ujerumani iliibuka kidedea kwa bao 7 kwa 0.