SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 11 Juni 2017

T media news

Kumbe Lesotho waliandaa mtu maalum wa kumlinda Samatta!!

Mbwana Samatta ameendelea kuwaumiza vichwa makocha wa timu za Afrika kufikiria njia na mbinu za kumdhibiti ili asifanye yake uwanjani na kusababisha madhara kwenye nyavu zao.

Kocha wa Lesotho Moses Maliehe amekiri kwamba, alikuwa anajua Tanzania inamchezaji anaecheza soka la kulipwa Ubelgiji na alikuwa akifikiria namna ya kumdhibiti na kuamua kumpa jukumu hilo mchezaji wake mmoja kuhakikisha Samatta hachezi kwa uhuru na kuwa mwiba kwa upande wao.

“Tulijifunza kutoka kwenye video za michezo ya Tanzania dhidi ya Nigeria pamoja na Botswana, tulikuwa tunajua ni timu nzuri yenye mchezaji professional anaecheza Ubelgiji ndio maana tulimpa jukumu namba sita wetu la kumkabili. Hata ukiangalia alifunga kwa mpira uliokufa, hakufunga kwa mipango iliyoandaliwa na timu.”

Licha ya kocha huyo kutoa jukumu la kwa mchezaji wake mmoja kuhakikisha anamzima Samagoal, lakini bado nahodha huyo wa Stars ali-shine na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini hazikuweza kutumiwa vyema kupachika mipira kambani.