Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Vyuo Vikuu nchini kwa mwaka wa masomo 2017/2018 watatumia mfumo mpya wa udahili tofauti na ule uliozoeleka wa kuchaguliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Haya yamebainishwa katika taarifa ya TCU iliyotolewa juzi ambapo imesema kuwa wanafunzi wote wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 watatumia mfumo mpya ambao unawataka kwenda vyuoni moja kwa moja kuomba nafasi.
Hivyo,taarifa hiyo imewataka wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kuomba nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu moja kwa moja vyuoni kuanzia tarahe 22 Julai 2017 hadi 13 Agosti 2017.
Sifa za kujiunga kwa wanafunzi wote ni kama ifuatavyo…
==> Isome taarifa ya TCU hapo chini