SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 6 Mei 2017

T media news

Sababu 5 kwanini mvuto wa mechi ya Arsenal na Manchestet unapungua

Siku ya Jumapili kuna pambano la kukata na shoka katika uwanja wa Arsenal Emirates, Arsenal watakuwa nyumbani kuwakaribisha Manchester United. Takwimu zinaonesha upinzani kati ya Arsenal na Manchester United unaoungua siku hadi siku huku zifuatazo zinaonekana kuwa sababu za upinzani huo kupungua.

1.Pesa za Kirusi. Mwaka 2003 tajiri wa Kirusi Roman Abromovich aliinunua rasmi klabu ya Chelsea, kabla ya hapo Chelsea walikuwa wakionekana wakawaida sana na United na Arsenal walikuwa watawala lakini pesa za Abromovich zimeleta mapinduzi ya soka na Chelsea kuonekana mpinzani sana hali iliyopelekea mechi kati ya Arsenal na United siku hizi inaonekana sio kali kama Chelsea na United.

2.Pesa za kiarabu. Baada ya Mrusi kuleta pesa zake Epl, baadae waarabu walimjibu na kuwekeza pesa zao katika klabu ya Manchester City, City nao kama ilivyo kwa Chelsea wakaanza kuleta upinzani mkubwa kwenye ligi kiasi cha kuanza kukaa juu ya Arsenal na Manchester United, hii kidogo ikaanza zipoteza Arsenal na United kwenye mbio za ubingwa na hata mvuto wao ukapungua.

3.Kustaafu kwa Alex Ferguson. Ni kweli vita ya Mourinho na Wenger inaifanya mechi hii kuwa na mvuto lakini uwepo wa Alex Ferguson kwenye benchi la Manchester United uliifanya mechi hii kuwa na mvuto zaidi, Ferguson alikuwa mshindani haswa na asiyependa kufungwa na timu za juu na hii iliifanya mechi hii kuwa ngumu sana na yenye mvuto.

4.Sio tena wapinzani wa makombe. Zamani kabla ya mwaka 2007 klabu hizi mbili zilikuwa zikipigana vikumbo kileleni, mara nyingi mechi zao huwa zinatoa taswira ya ubingwa kama sio wa FA baasi wa EPL lakini sasa kama mechi hii ya Jumapili Arsenal yuko nafasi ya 6 na United yuko nafasi ya 7 haina athari yoyote katika mbio za ubingwa.

5.Kuondoka kwa Patrick Viera na Roy Keane. Viungo hawa wawili walikuwa wakifanya mechi hii kuwa na mvuto, vyombo vya habari vingi vilikuwa vinaisubiri mechi hii ili kuona Roy Keane na Patrick Viera watafanya kitu gani, baada ya wawili hao kuondoka kwa sasa timu hizi zinakosa wachezaji wenye kuifanya mechi hii kuonekana ya upinzani mkubwa kama zamani kipindi wapo