SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 6 Mei 2017

T media news

Lioneil Messi anavyompa changamoto Cristiano Ronaldo katika Champions League

Cristiano Ronaldo anatajwa kama mfalme wa Champions League kutokana na mambo anayoyafanya katika mashindano hayo, lakini upande wa pili wa Lioneil Messi hawakubali hili wakidai nyota wao ni bora kuliko Mreno, leo tuone baadhi ya ubora kati ya nyota hawa wawili.

Mabao. Wanasema mpira ni magoli sasa Cristiano Ronaldo anaongoza katika ufungaji katika mashindano hayo, hadi sasa ana mabao 103 ambayo ameyafunga katika michezo 138, ambapo mashabiki wa Lioneil Messi wanakataa kusema Ronaldo anafunga kuliko Messi kwani Lioneil Messi ana mabao 94 ambayo kayafunga katika michezo 115 ambayo ni michezo 23 pungufu ya Ronaldo, wanaamini Messi angecheza michezo sawa na Ronaldo angefunga mabao zaidi ya 103 hadi sasa.

Wastani wa dakika kwa kila bao. Mabao ambayo Cristiano ameyafunga hadi sasa ni 103 lakini inaonekana Mreno huyo anatumia mda mrefu sana kufunga kuliko Lioneil Messi kwani Ronaldo huwa inamchukua dakika 116 kufunga bao moja wakati Lioneil Messi yeye huwa inamchukua dakika 101 tu kufunga bao moja.

Jinsi walivyofunga mabao yao. Mashabiki wa Messi wameibuka na jina la utani wakimuita Ronaldo “Penaldo” wakimaanisha anafunga magoli mengi ya penati na jedwari la ufungaji wao linaonesha Cristiano Ronaldo magoli yake 22.3% ameyafunga kupitia freekicks na penati huku 77.3% akifunga kawaida, lakini Lioneil Messi amefunga mabao yake 13.8%tu amefunga kwa freekick na penati huku 86.2% akifunga kawaida.

Assists. Ronaldo anaonekana ana mchango mkubwa kwa Real Madrid katika assists kwani katika michezo aliyocheza kila baada ya dakika 362 alitoa assist huku Lioneil Messi akichukua mda mrefu kidogo kutoa assist kwani ametumia mda mrefu kidogo kutoa assists kwani ametumia dakika 381 kutoa assists.

Misimu waliyoibuka vinara wa ufungaji. Hapa pia Ronaldo na Lioneil Messi wako sawa ambapo wote hadi sasa wamekuwa wafungaji bora wa UCL kila mmoja kwa misimu mitano, kiujumla nyota hawa wote wanaonekana ni bora katika michuano hii japokuwa Cristiano Ronaldo anaonekana bora zaidi msimu huu ila Messi kwa upande mwingine anaonekana bora sana.