SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 6 Mei 2017

T media news

Balotelli amjibu Brenden Rodgers kupitia Twitter.

Mario Balotelli amekuwa na msimu mzuri sana toka ajiunge na klabu ya Nice ya Ufaransa, wikiendi iliyopita akiisaidia Nice kuisimamisha PSG ambao wako katika mbio za ubingwa wa Ufaransa msimu huu.

Lakini nje ya uwanja Balotelli ambaye Jumatano alionekana akifuatilia kwa karibu nusu fainali ya Champions League kati ya Monaco na Juventus amekuwa haishiwi visa, matukio na vituko vya kila aina.

Wiki hii kocha wa Celtic Brenden Rodgers ambaye ndiye akimsajili Balotelli kwenda Liverpool aliongea kauli moja ya utani, lakini kauli hio ilionekana kama dhihaka kwa Baloteli badala ya utani.

Rodgers aliulizwa ni mchezaji gani bora ambaye ameshawahi kumfundisha au kukaa nae mazoezini ambapo huku akicheka alijibu “nadhani Balotelli alikuwa mchezaji mzuri sana” akaendelea kucheka.

Mbaya zaidi wakati Rodgers akiendelea na mazungumzo alivuka mipaka na kusema yeye hakutaka kumnunua Balotelli bali kamati ya usajili ya Liverpool ndio ambayo ilimleta mchezaji huyo klabuni hapo.

Kusikia hivyo Balotelli hajuweza kukaa kimya bali alikimbia moja kwa moja Twitter na kuandika huku akicheka “Brenden Rodgers wewe ni kocha bora nilyewahi kukaa naye” kisha akaweka emoji za kucheka.