Toka apewe nafasi na kocha aliyepita Louis Van Gaal Marcus Rashford amekuwa katika kiwango kizuri na sasa hadi Jose Mourinho amekuwa akimuamini.
Umri wake ndio kwanza ni miaka 19 lakini nguvu pamoja na kasi yake uwanjani mara nyingi vimekuwa vikiwapa sana tabu mabeki wa timu pinzani.
Rashford anaonekana na njaa ya magoli sana lakini sasa imebainika kumbe Rashford sio njaa tu ya magoli bali ana njaa sana yenyewe yenyewe na kila saa huwa anakula kula.
Kwa siku Rashford amekuwa akila mara sita lakini kupika kwake kumekuwa tatizo na hivyo magari maalum ya misosi yamekuwa yakipiga hodi getini kwake mara sita kila siku.
Nourish Fit Food ambao huwa ndio wanampelekea misosi Rashford wanasema Rashford hanaga chakula maalum na kila siku amekuwa akipelekewa misosi tofauti.
Lakini msemaji wa Nourish amesema “Rashford mara nyingi amekuwa akisafiri sana na timu kwahiyo vyakula tunavyompelekea vinasaidia kuuweka mwili wake sawa na kujenga misuli”
Lakini Rashford asubuhi subuhi akiamka ni lazima apige uji na asubuhi hiyo tena ataletewa mayai baada ya muda na anapenda pia kuku waliochanganywa na mboga za majani na viazi vitamu pia.
Misosi ya Rashford imekuwa ikimgharimu kiasi cha £50 kwa siku na hii inamaanisha kwa mwezi Rashford hutoa kiasi cha £500 kutoka katika mshahara wake wa £50,000 anaopokea kila wiki.
Manchester United ni tofauti na vilabu vingine ambavyo huajili watu kwa ajili ya misosi ya wachezaji kwani wao hawana mtu wa moja kwa moja bali muda mwingi wanamuita Mark Ellison ambaye pia ndiyo anaangalia suala la vyakula la bondia Anthony Joshua.