SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 18 Mei 2017

T media news

Juventus wabeba ndoo, Madrid akaribia ubingwa,United sare kama kawa.

Juventus imekuwa timu ya kwanza nchini Italia kushinda makombe ya Coppa Italia mara 3 mfululizo baada ya ushindi wa bao 2 kwa 0 dhidi ya Lazio.

Juventus ambao wanakabiliawa na mchezo wa fainali ya Champions League mwezi ujao walifanikiwa kupata magoli yao kupitia beki Dani Alves na Leornado Bonucci na kuwapa ubingwa mwingine wa Cippa Italia.

Wapinzani wa Juventus katika fainali ya Champioms League timu ya Real Madrid nao wamekaribia ubingwa wa La Liga baada ya kuibamiza Celta Vigo kwa bao 4 kwa moja.

Magoli mawili ya Cristiano Ronaldo na moja moja kutoka kwa Toni Kroos na Karim Benzema yaliifanya Madrid kuipita rekodi yao ya mabao ya ugenini waliyoiweka msimu wa mwaka 2014/2015 ya kufunga mabao 53 baada ya hapo jana kufikisha 54.

Baada ya matokeo hayo sasa Real Madrid itawabidi kupata hata suluhu tu katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Malaga ili kuweza kutawazwa kama mabingwa wapya wa La Liga msimu huu.

Huko Uingereza Manchester United walitoka sare na kuufanya msimu huu kuwa msimu ambao wamepata ushindi mara chache katika ligi kuu wakiwa hadi sasa wameshinda mara 17 tu.

Mchezo huo dhidi ya Southampton ulimshuhudia Michael Carrick ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea West Ham akicheza mchezo wake wa 700 toka ajiunge na mashetani hao wekundu.