Hakika ni mchezaji tishio, hakika anapaswa kufananishwa na Thiery Henry na hakika Kylian Mbape anastahili kuuzwa zaidi ya £100m kama inavyotajwa na Monaco.
Usiku uliopita Mbape ambaye amekuwa na msimu mzuri sana ilimchukua dakika 19 tu kuzifumua nyavu za St Ettiene kwa kufunga bao la kwanza na likiwa ni la 15 kwake katika msimu huu.
Bao la pili lilifongwa na Valere Germain dakika ya 90 liliuzamisha utawala wa Paris Saint German utawala ambao ulidumu kwa miaka minne katika ligi hiyo ya Ufaransa.
Monaco ambao wiki iliyopita walitolewa katika michuano ya Champions League hili ni kombe lao la kwanza la ligi ndani ya miaka 16 kwani mara ya mwisho walilichukua mwaka 2000.
Kwa matokeo hayo ya Monaco wamefanya kile walichofanya Juventus ndani ya usiku mmoja kwani Juve nao wakati Monaco wakitwaa ubingwa wa Ufaransa wao walikuwa wakitwa ubingwa wa Copa Italia usiku huo huo.
Sasa Monaco ambao hadi sasa wamecheza michezo 37 wanakuwa na alama 92 kileleni alama ambazo hata PSG wakishinda mchezo wao wa mwisho hawawezi zifikia.