SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 3 Mei 2017

T media news

Kesi ya Wema Sepetu Kutumia BANGI Yapigwa Kalenda


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeambiwa kwamba upelelezi wa kesi ya kukutwa na bangi inayomkabili Muigizaji maarufu, Wema Sepetu na wenzake umekamilika.

Hatua hiyo imefikiwa   ambapo upande wa Jamhuri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema kwamba upelelezi umekamilika dhidi ya msanii huyo na wakili wa Serikali Helleni Mushi aliomba kesi hiyo kuarishwa  na kupangwa tarehe ya kuanza kusikilizwa ili watuhumiwa waanze kusomewa maelezo ya awali.

Katika kesi ya msingi, Wema anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. 

Mbali na Wema washitakiwa wengine ni wafanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa (21) na Matrida Abas (16), ambapo wote wanashtakiwa kwa kosa moja la kukutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda kosa hilo Februari 4 mwaka huu, nyumbani kwao Kunduchi Ununio , Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.

Hakimu Simba alisema  kesi hiyo itaanza kusikilizwa, Juni Mosi, mwaka kwa watuhumiwa kuanza kusomewa maelezo ya awali.