SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 23 Mei 2017

T media news

JINSI Utawala wa Magufuli Ulivyowaumbua Wanahabari Makanjanja, Wengi 'Wamepotea'...!!!


Sasa ni dhahiri shahiri wanahabari wengi makanjanja wamekuwa na maisha magumu sana kwani wengi walitegemea kuishi kwa kuwasifia 'wanasiasa' na 'wapiga dili'. Mathalani, Ma-don wakubwa wa unga,makontena nk walikuwa wanamiliki kundi la waandishi wa habari wenye lengo moja kuu tu 'kuwasafisha'.

Hali imegeuka, magenge mengi yameyeyuka huku wakiwaacha vijana wao (waandishi makanjanja) wasijue cha kufanya. Kundi kubwa la makanjanja kwa sasa limegeukia mitandao ya kijamii kutengeneza akaunti feki zenye mrengo wa kupotosha. katika pitapita zangu nimekutana na baadhi ya wahariri ambao kabla ya Manji kubanwa walikuwa wenye 'fujo' nyingi mjini lakini ghafla hali yao imedhohofu. Udhibiti wa posho kwa wanasiasa pia umesababisha waandishi wengi kukosa ujira kwani hakuna mwanasiasa anayemudu kubeba waandishi kwa kukosa pesa za kuwalipa.

Magazeti mengi yaliyotamba miaka mitano iliyopita yamekufa au yanatoka mara moja moja sana, huku gazeti la Jamvi la habari likitokomea kusikojulikana.

Ushauri wangu ni kwamba kundi hili la 'wapambe' na 'makanjanja' wa habari sasa waelekeze nguvu zao katika mambo yenye tija kwa ajili yao binafsi na kwa taifa kwani kwa sasa hata zile kurasa zao maarufu zenye kukejeli serikali katika mitandao ya kijamii zimedorora.

Heshima imerudi mjini.

Credit - Jf