SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 10 Mei 2017

T media news

Breaking: Matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa CHADEMA Bunge la Afrika Mashariki



Bunge la Tanzani leo limepiga kura na kuwachagua wabunge wawili wa CHADEMA watakaoungana na wenzao 7 kutoka CUF na CCM kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Uchaguzi huo wa wabunge wa CHADEMA umerudiwa leo baada ya wagombea wa kwanza kukataliwa bungeni kwa kupigiwa kura ya hapana kwa kile kilichoelezwa kuwa hawakuwa wamekidhi vigezo.
Katika uchaguzi wa leo, wabunge wawili waliochaguliwa ni  Josephine Sebastian Lemoyan na Pamela Pamela Maasay.
Katika kinyang’anyiro hicho wagombea wengine walikuwa nia Ezekiel Wenje, Lawrence Masha, Salum Mwalimu na Prof. Safari.
Kufuatia ushindi wa wagombea hao wawili, wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki sasa wanafikia 9 ambapo 5 ni wanawake na 4 ni wanaume.
Wabunge tisa wa Tanzania katika Bunge las Afrika Mashariki ni;
 Fancy Nkuhi (CCM)Happiness Legiko (CCM)Maryam Ussi Yahya (CCM)Dkt Abdullah Makame (CCM)Dkt Ngwaru Maghembe (CCM)Alhaj Adam Kimbisa (CCM)Habib Mnyaa (CUF)Josephine Sebastian Lemoyan (CHADEMA)Pamela Pamela Maasay (CHADEMA).

Matokeo : Kura zilizopigwa 296  

Kura halali 296 

Abdallah Safari 35

Wenje 34

Josephine Lemoyan 219

Lawrence Masha 44

Pamela Maasay 200 

Salim Mwalimu 59

Hayo ndo matokeo

Mshindi ni Josephine Leyamon