Shirikisho la soka nchini TFF limefafanua kuhusu sintofahamu iliyotawala baada ya taarifa kuenea kwamba TFF imeisadia Yanga kurudi nchini baada ya msafara wa watu 12 kukwama kutokana na kuachwa na ndege waliyopanga kurudi nayo.
Wadau wa soka wamekuwa wakidhani kwamba, huenda TFF imetoa pesa ili kuwalipia wachezaji 11 pamoja na katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa ili warudi nchini.
Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema wamelazimika kufanya hivyo ili kutovuruga ratiba ya michezo ya ligi kuu Tanzania bara pamoja na ile ya kombe la shirikisho ambapo Yanga inatarajia kucheza dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa FA Cup April 22, 2017.
“Ukizingumzia mechi za vilabu za kimataifa TFF lazima itimize wajibu wake kwa sababu ni taasisi yenye mamlaka ya kufuatilia mchezo wa mpira wa miguu. Lilipojitokeza suala la Yanga kuachwa na ndege, kumbuka hapa kuna ratiba mbalimbali zinazoihusu Yanga kucheza, sasa TFF ilichokifanya ni kumuuliza mkuu wa msafara Bw. Sanga ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Ruvuma akatuelezea vizuri tatizo ni nini.”
“Akatuambia Yanga tayari wamejipanga kurudi tarehe 20 April, 2017 na terehe 22 wanamchezo wa FA Cup (Azam Sports Federation Cup) bahati nzuri sisi tunamawasiliano mazuri na shirika la ndege la Emaretes ambao walituambia wao wana ndege ya inayoondoka tarehe 17 jioni na inanafasi kwahiyo tukawaambia Yanga wafanye taratibu za kubadilisha tiketi zao kutoka shirika la ndege la Uturuki kwenda Emirates wakakubali na sasa wapo njiani kurejea nyumbani.”
“Kwa hiyo tuliamua kuwasaidia kuratibu katika hilo ili kuwaweka sawa kisaikolojia ila hatujatoa pesa kuwalipia nauli Yanga.”