Na Zainabu Rajabu
YANGA yapiga hodi katika uongozi wa Mbeya City kwa kutaka kumsajili kiungo wao Kenny Ally ambae mkataba wake utafikia tamati mwishoni mwa msimu.
Kiongozi mmoja mwenyewe ushawishi mkubwa ndani ya klabu ya Yanga ameithibitishia shaffihdauda.co.tz kuwa klabu hiyo inahitaji saini ya nahodha huyo wa City na wanaangalia uwezekano wa kumsajili baada ya kumalizika kwa msimu huu kutokana na kiwango kikubwa alichoonyesha siku za hivi karibuni.
Shaffihdauda.co.tz. ilimtafuta Kenny Ally kutaka kujua kama ana taarifa zozote kuhusiana na mabingwa hao kutaka saini yake kwa ajili ya msimu ujayo ambapo alisema, hana sababy ya kutokujiunga Yanga kama watampatia kiasi cha shilingi milioni 50 atakuwa tayari kuitumikia klabu hiyo.