Jukwaa la Wahariri Tanzania leo limetangaza rasmi uamuzi utakaotekelezwa mara moja na Vyombo vyote vya Habari wa kutofanya kazi na RC Makonda, ambapo uamuzi huo umeenda sambamba na kauli ya kwamba atakaye shirikiana naye atajumuishwa kama adui wa Uhuru wa Habari nchini.