Mchungaji wa Kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima ameyasema hayo mapema hii leo alipokwenda kukitembelea kituo cha Clouds Media kwa lengo la kuwapa pole na kuwatia nguvu wanafamilia wa Clouds Media.
Amesema kazi yake aliyoagizwa na Mungu ni kuwasemea watu na hivyo hatosita kuwasemea watu kwakuwa asipofanya hivyo mwisho wa siku miti na mawe itasimama kumuuliza.
Kuhusu Jambo la Mtoto anayedaiwa kuwa Wakwake, amesema hizo zilikuwa ni njama za kumchafua kwahivo madai hayo si ya kweli ambapo ameweka wazi kuwa ana watoto wa tatu pekee ambao sio wa nje ya ndoa, Pia Gwajima amearifu kuwa bnti huyo alilishwa maneno asema kuwa amezaa nae, yupo ustawai wa jamii akiandika maelezo kuwa maneno aliyotoa niya uongo.
Hata hivyo Gwajima ameweka wazi kuwa hana ugomvi na Serikali tiliyopo madarakani