NAHODHA WA SIMBA, JONAS MKUDE.
NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude, amesema mzuka wa kutaka kuchukua makombe mawili unazidi kuwapanda kichwani wachezaji wa timu hiyo na wamepania kutimiza lengo hilo.
Akizungumza na Nipashe jana, Mkude alisema ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye mchezo wao wa robo fainali dhidi ya Madini FC ya Arusha Jumapili iliyopita, umewafanya kuona wanakaribia kutimiza ndoto hiyo.
"Hiki ndicho kitu ambacho kipo akilini mwetu, tutapambana kuona tunafikia malengo na ndoto yetu ya kutwaa makombe mawili msimu huu, nia hiyo tunayo," alisema Mkude.
Alisema changamoto iliyopo mbele yao kwa sasa ni michezo yao ya Kanda ya Ziwa ambayo wanaamini kama watafanikiwa kufanya vizuri watakuwa wameukaribia ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Wakati wakiwa wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa tofauti ya pointi mbili, Simba tayari imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (FA)