Imebainika kuwa njama za kumtoa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda zilianza Bungeni kwa kuratibiwa na baadhi ya wabunge wanaohusishwa na mtandao wa dawa za kulevya.
Katika kudhibitisha hili, walifanya kikao Dodoma kilichohusisha baadhi ya wabunge na kukubaliana kuunganisha nguvu na wafanyabiashara na Viongozi wa Dini waliohusishwa na biashara ya Dawa za kulevya.
UTEKELEZAJI WAKE :-
1. Walikubaliana kuungana na baadhi ya viongozi wa ukawa ambao hapo awali walikuwa mahasimu wao kisiasa, zoezi lililoratibiwa na mbunge mmoja ambae ni mtoto wa kiongozi mstaafu, rejea picha za matukio mbalimbali wakati wa mechi ya simba na yanga (zoezi lilifanikiwa)
2. Kuwaunganisha kwenye mtandao wafanyabiashara wakubwa waliotajwa na Makonda pamoja na kumuunganisha Askofu mmoja alietuhumiwa kujihusisha na mtandao wa dawa za kulevya, lengo la kuwaunganisha hawa ni kupata ufadhili wa fedha za kutosha, rejea kauli za baba askofu akidhibitisha kujizatiti kumuondoa Makonda Dar (zoezi lilikamilika)
3. Kushawishi marafiki wakubwa wa makonda ambao walikuwa wakimsaidia Makonda katika vita ya dawa za kulevya kwa kuwarubuni kumgeuka makonda na kuungana katika kambi yao kwa makubaliano kuwa makonda akiondoka Dar watashinikiza kupatikana kwa mkuu wa mkoa ambae atakuwa hana purukushani za dawa za kulevya, udhibitisho wa hili ni RUGE KUMGEUKA MAKONDA(zoezi limefanikiwa)
4. Kutumia baadhi ya mawaziri ambao watu wao walijeruhiwa kwenye kampeni za uchaguzi na kuwaingiza kwenye mtandao wa kumtoa Makonda Dar, ushahidi wa hili ni alliance ya Mgombea wa Urais kutoka Lindi, mahusiano yake na waziri ambae amejitoa Muhanga kumpinga Makonda hadharani.(zoezi lilikamilika tangu dodoma)
5. Kutengeneza tukio ambalo litamfanya makonda apate aibu mjini, kisha wamtake makonda aaibike, wakishapanga mtego mmoja makonda akaujuaga mida ya nyuna akukwepa, sasa hili tatizo la makonda kwenda CLOUDS usiku lilivyotokea wakaamua KUKANYAGIA HAPO HAPO.
6. Kuwashawishi baadhi ya wabunge wa chama tawala kutoa vitisho kama Makonda hataondolewa kwenye ukuu wa mkoa basi watajiuzulu , ushahidi wa hili ni post ya face book ya mhe Kingu(zoezi lilifanikiwa)
HITIMISHO
-Jiulize tangu lini clouds na mmiliki wa ipp walishakuwa na mahusiano ya karibu kama juz?
- Jiulize tangu lini EFM na CLOUDS walishakuwa marafiki?
- Jiulize tangu lini Askofu alishawai kukaa karibu na CLOUDS?
- Jiulize tukio linalotajwa la uvamizi limetokea ijumaa, kelele zimeanza kupigwa Jumatatu hii ni baada ya hawa mabwana kukutana jumamosi na kufanya kikao cha pamoja jumaosi na jumapili hela ikatoka kanisani kwa askofu kwa kazi maalum Jumatatu.
-Jiulize hiyo jumatatu jamaa kafanya mahijiano live asubuhi, kisha saa nne asubuhi Mhe waziri anatinga CLOUDS akiwa na mzee wa ipp, na hapo hapo kamati ya huduma za bunge inakwenda CLOUDS mchana huo huo?
-Jiulize kwa nini wote wameshinikiza Makonda aondolewe Dar?
Na mwisho kabisa, baada ya Mhe Rais Dkt. John Magufuli kustukia njama zao kutokana na kuwa na kikosi imara cha ujasusi katika maeneo mbalimbali akawabomoa LIVE bila chenga pale ubungo wakati wa uzinduzi wa mradi wa flyover.
TUKIDHANI WATAMUELEWA MHE RAIS WAMEGOMA NA KUMSHAWISHI MHE WAZIRI KUUNDA KAMATI WAKATI WANAJUA MHE RAIS AKISHAONGEA MJADALA UMEKWISHA, LAKINI WAO WAMEAMUA SASA KUPAMBANA NA NGUVU ZA MHE RAIS KWA KUSHINIKIZA BAADHI YA WABUNGE WAJIONDOE KWENYE NYADHIFA ZAO.
NB:Hayo ni Maoni ya Mmoja wa Msomaji Wetu na Wla Si Msimamo wa Blog Hii,Sisi Kazi Yetu ni Kufikisha Taarifa Tu,na Hata Wewe Unaweza Kuwasiliana nasi kuweza Kuandika Makala ya Maoni Yako Hapa