SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 5 Machi 2017

T media news

Raisi Magufuli: Hata mkeo anaweza asikupende siku nyingine, cha muhimu ni kuchapa kazi

Rais Magufuli leo mkoani Mtwara wakati akiweka jiwe la msingi katika kituo cha kupooza umeme njia ya KV 132 amelipongeza Shirika la Umeme nchini Tanesco na kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini, kwa juhudi zake katika kazi.

Rais Magufuli amesema aliamua kumteua Sospeter Muhongo kuwa Waziri kutokana na ukweli kwamba alikuwa anaona uchapaji wake wa kazi kipindi ambacho yeye ni Waziri wa Ujenzi.

"Lengo lililokuwa kwenye ilani ya Uchaguzi kwa mwaka jana ilikuwa asilimia thelathini na kitu nyinyi mkafika mpka asilimia arobaini, na sasa hivi mko zaidi ya asilimia 46 sasa nisipowapongeza nitakuwa mtu mbaya wa moyo mbaya.

" Na mimi na moyo mzuri kweli ndiyo maana nawapongeza wizara pamoja na Tanesco haya matatizo mengine ambayo yanatokea ni kwa sababu tuliingia mikataba ya hovyo huko nyuma, ya kulipia capacity charges ninajua mnayashughulikia na tunajaribu kutafuta pesa za mikopo tulipe haya madeni twende na Tanesco mpya" alisema Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli alimsihi Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo

"Nilipoteuliwa kuwa Rais sikuona mtu mwingine anayefaa kama Muhongo, nikamrudisha hapa hapa sababu mimi nilipokuwa nikihesabu kilometa za barabara yeye alikuwa anaesabu kilometa za nyaya, kwa hiyo nilifahamu kazi yake na saa zingine ukifanya kazi vizuri unakuwa kama hupendwi pendwi hivi, lakini kwa nini wakupende? Hata mke wako anaweza asikupende siku zingine, wewe chapa kazi" alisisitiza Rais Magufuli

Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa katika maisha ya kila siku huwezi kupendwa na kila mtu

"Hata ndugu yako anaweza asikupende, saa zingine hata baba yako au hata mdogo wako anaweza asikupende, huwezi ukapendwa na kila mmoja, hata mitume hawakupendwa na wote na wengine walisulubiwa pamoja na kwamba walifanya mazuri. 

"Kwa hiyo Prof. Muhongo wewe fanyakazi tena usihangaike hata kusoma ile mitandao, mimi sisomagi hiyo mitandao achana nayo watandae huko huko wenyewe wewe chapa kazi" alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.