SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 20 Machi 2017

T media news

Mzimu wa Ranieri bado unawatesa Leicester City.

Claudio Ranieri ndiyo kocha ambaye aliwapa Leicester kombe katika msimu uliopita, Ranieri aliwapa Leicester kombe katika mazingira ambayo hakuna mtu aliyetarajia kwani ilionekana wazi ni ngumu kwao.

Baada ya Claudio Ranieri kuwapa kombe Leicester msimu uliofuata mambo yalionekana kumwendea kombo, Leicester walionekana kuyumba sana na hata kufikia hatua ya kutaka kushuka daraja.

Mabosi hawakumvumilia, mabosi wakasahau yote aliyowafanyia, wakajishaulisha kuhusu ubingwa wakamtimua. Kutimuliwa kwa Ranieri kuliibua mjadala mkubwa sana wengi wakisema ameonewa.

Baada ya kumtimua, Leicester walianza mchakato wa kumtafuta kocha mpya. Inasemekana sasa dhambi ya kumtimua Ranieri ikaanza kuwatesa katika mchakato huu wa kumtafuta kocha mpya.

Makocha wengi wakubwa waliona hawawezi jiunga na klabu ya Leicester kutokana na walichomfanyia Ranieri.Mmoja wa makocha hao ni Casseri Prandelli kocha wa timu ya taifa ya Italia.

Prandelli ameweka wazi kwamba mabosi wa Leicester City walimfuata wakimtaka achukue mikoba, lakini alipokumbuka kilichomtokea kocha wa Leicester City bwana Claudio Ranieri, Prandelli alisema hapana.

“Walipokuja tu nilisema hapana, huwezi ukachukua kazi namna hiyo, utaendaje kuwa kocha wa Leicester kutokana na kile alichofanyiwa Ranieri msimu uliopita?” alisema Prandelli.

Prandelli anasema yeye aliogopa kilichomtokea Ranieri, Prandelli anaamini Ranieri ni kati ya makocha wakubwa na anaowaheshimu duniani na hakupaswa kufanyiwa alichofanyiwa na Leicester City.