Viongozi wa Kamati ya Bunge, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni serikali kuingilia majukumu yao.
Viongozi hao wamendika barua na kuzituma kwenda Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kueleza uamuzi huo walioamua kuuchukua leo.