SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 20 Machi 2017

T media news

Zitto Kabwe: Wanahabari suseni kuandika habari zote za serikali

Baada ya kauli iliyotolewa na Rais Dkt Magufuli leo akimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalaam, Paul Makonda kuendelea na kazi na kuachana na habari zinazoandikwa mitandaoni, viongozi na wananchi wamejitokeza na kuonyesha kusikitishwa kuhusu uamuzi huo.

Kwa siku kadhaa zilizopita wananchi walikuwa wakishinikiza RC Makonda ajiuzulu au mamlaka husika itengue uteuzi wake baada ya kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwamo za kuvamia kituo cha habari cha Clouds Media Group usiku akiwa na Askari wenye silaha, vitendo vya rushwa.

Tuhuma nyingine na kutumia cheti cha mtu mwingine baada ya kufeli kidato cha nne na pia kuwa na utajiri ambao hauendani na kipato chake.

Akiwa katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya juu Ubungo Dar es  Salaam, Rais Dkt Magufuli alisema wakazi wa Dar es Salaam  wamekalia udaku ambao hauwasaidii kuleta maendeleo huku wengine wakiingilia uhuru wake na kumpangia cha kufanya.

Kauli ya Rais Magufuli kuhusu RC Makonda “kusemwa” mitandaoni

Kufuatia kauli hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameandika;

Mkuu wa Mkoa anavamia chumba cha habari binafsi Kwa mitutu ya Bunduki na Askari wa Umma. Wananchi wanalalamika kuhusu uvamizi huu ikiwemo Waziri, Wabunge, Wamiliki Wa vyombo vya habari na waandishi wenyewe.

Rais bila kumung’unya maneno anatamka hadharani kuwa Mkuu wa Mkoa aendelee na kazi zake. Hii maana yake ni kwamba Rais amemtuma Mkuu wa Mkoa kuvamia Chombo cha habari.

Nawashauri wana habari wote kukutana kupitia MOAT, Jukwaa la Wahariri na Press Clubs na kuamua Kwa pamoja kususia kuandika habari zote za Serikali mpaka hapo Serikali 1) itakapolaani tukio hili na kuahidi kuwa halitotokea tena 2) itakapochukua hatua kali dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam.

Nakumbuka Sana Jukwaa la Wahariri chini ya Sakina Dewji-Datoo.