SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 27 Machi 2017

T media news

Majibu Kwa Diallo Kuhusu Alichojifunza Kwenye Sakata la Paul Makonda


Nimesoma andiko la Mbunge wa zamani wa Ilemela Mhe.Dr.Anthony Dialo kuhusu sakata la Makonda kuvamia studio za Clouds, kutetewa na JPM, Nape kuunda Kamati na yaliyomkuta Nappe baadae.

Katika taarifa hiyo ya Diallo anaeleza mambo kadhaa aliyojifunza kutokana na mikasa hiyo yote. Pamoja na mambo mengi anayodai amejifunza naorodhesha machache;

1. Amesema amejifunza kuwa Makonda ni kiongozi shupavu tangu akiwa Rais wa shirikisho la vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO). 2. Amesema amejifunza kuwa hakuna vyama vya upinzani Tanzania.

3. Anasema amejifunza vyama vya upinzani vimepoteza dira.

#MAJIBU:

1. Mhe.Diallo inaonekana anaongea vitu asivyovijua vizuri. Makonda hajawahi kuwa Rais wa shirikisho la vyuo vikuu Tanzania. However hakuna kitu kinachoitwa Shirikisho la vyuo vikuu Tanzania. Kuna Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania, ambayo kwa kifupi ndio TAHLISO. Na Makonda alikuwa Mwenyekiti sio Rais. TAHLISO haijawahi kuwa na kiongozi anayeitwa Rais. Msaidieni Diallo.

2. Diallo anasema hakuna upinzaninTanzania, halafu baadae anasema upinzani umepoteza dira. Kama upinzani haupo, huo uliopoteza dira umetoka wapi? Mbona anaongea na kujipinga mwenyewe? Msaidieni Diallo.

Huwezi kusema sina gari, halafu baadae useme gari yako imepasuka tairi. Kama huna gari hiyo iliyopasuka tairi imetoka wapi? Kuna haja ya somo la "Logic and argumentation skills" au "Critical Thinking" kuwa masomo ya lazima shuleni. Msaidieni Diallo.

3. Diallo anasema hakuna upinzani nchini wakati, aliyemgaragaza kwenye ubunge wa Ilemela mwaka 2010 na kumpoteza kwenye ramani ya siasa ni mpinzani. Highness Kiwia wa Chadema ndiye aliyemfanya Diallo mpaka leo yupo mtaani. Pengine angekua waziri muda huu, lakini Kiwia (mpinzani) akamng'oa kwenye ubunge. Leo anasema hamna upinzani?? Msaidieni Dialo.!!

By @malisa_gj