SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 22 Machi 2017

T media news

Bilionea Rockefeller Aliyejenga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Afariki Dunia..!!!


Bilionea maarufu nchini Marekani aliyefahamika zaidi kwa kutoa pesa kuwasaidia watu wasiojiweza sehemu mbalimbali za dunuia, David Rockefeller amefariki dunia akiwa usingizini nyumbani kwake Poncantico Hills, New York akiwa na umri wa miaka 101.

Kupitia Taasisi yake ya The Rockefeller Foundation  alifanikiwa kufadhili ujenzi wa majengo marefu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Rockefeller alikuwa mtoto wa mwisho kwenye familia watoto watano wa kiume wa John D Rockefeller Jr. Ndiye aliyekuwa mjukuu wa mwanzilishi wa kampuni ya Standard Oil John D Rockefeller.

Mzee huyo ndiye aliyekuwa anasimamia mali na biashara za familia hiyo, pamoja na miradi yake ya kusaidia jamii, ingawa hakuwahi kutafuta wadhifa wowote wa kisiasa, kaka zake wawili walihudumu serikali.

Nelson Rockefeller alifanya kazi kama gavana wa New York na kwa muda kama Makamu wa Rais wa Marekani huku Winthrop Rockefeller naye alikuwa gavana wa Arkansas.

David Rockefeller alihitimu kutoka chuo kikuu cha Harvard mwaka 1936 na kutunukiwa Shahada ya Uzamifu Katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Chicago mwaka 1940.

Alitumikia Jeshi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na baadaye akafanya kazi katika benki ya Chase Bank, ambayo baadaye ilikuwa benki ya JP Morgan Chase.

Bw Rockefeller alimiliki kazi za sanaa za thamani ya $500m (£404m).

Alipokuwa anasherehekea kutimiza miaka 100 mwaka 2015, alitoa ardhi ya ekari 1,000 kwa mbuga ya taifa katika jimbo la Maine.

Juhudi zake za kusaidia jamii zilimfanya kutunukiwa Nishani ya Uhuru ya Rais mwaka 1998.

Alikuwa na watoto wanne – David Jr, Richard, Abby, Neva, Margaret na Eileen. Mkewe Margaret (jina lake la kuzaliwa McGrath) alifariki 1996.