Kambi ya upinzani nchini Kenya imehairisha maandamano ya mtaani na badala yake imeamua kuweka mkazo katika kuwahamasisha wafuasi wao kujiandikisha katika daftari la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Katika mkutano wao uliohusisha vyama 15, viongozi wa vyama vya upinzani wamesema hawatatumbukia katika mtego wa chama tawala cha Jubilee wa kuandamana kupinga sheria ya uchaguzi iliyopitishwa na bunge na kutiwa saini na Rais Uhuru Kenyatta.
Wakati huo huo, kiongozi wa upinzani nchini humo Rais Odinga, amemshutumu bila kumtaja jina, aliyewahi kuwa waziri nchini humo kwa kuendesha kile alichokiita mchezo mchafu katika zoezi la uandikishaji wapiga kura, ambapo amesema kuwa katika zoezi hilo kuna majina kuna vitambulisho vingi bandia (vitambulisho vya wapiga kura hewa) vinatengenezwa, ikiwa ni pamoja na kuandisha watu wasio raia
"Leo tuko hapa kudhihirisha kuwa IEBC inaandikisha watu wasio raia wa Kenya kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa mezi Agosti, 2017" Amesema Odinga huku akionesha namba za vitambulisho 19 vya watu anaodai kuwa hawana sifa