Shinyanga. Mbunge wa Shinyanga, Stephen Masele amewataka viongozi kuzungumza ukweli kuhusu njaa na kuacha kuogopa kutumbuliwa.
Masele amesema hayo jana wakati akitembelea kata mbalimbali za jimbo hilo ili kupokea kero za wananchi na kuzifanyia kazi.
Ameitaka Serikali kutambua kuwa wananchi wana njaa na hakuna chakula huku akiomba kilicjopo kuuzwa kwa kwa bei nafuu.
“Maeneo yote niliyopita nimekutana na vilio vya wananchi wakiomba msaada wa chakula kutokana na baadhi yao kudai wanakabiliwa na uhaba wa chakula na bei kubwa.
“Rais John Magufuli anaomba tumsaidie, na sisi tunamsaidia kwa kumwambia ukweli kuwa wananchi wana njaa watendaji wa Serikali hawasemi ukweli kwa hofu ya kutumbuliwa,” alisema Masele.