Kwa hili la Madawa Mastaa wengi bongo watakosa usingizi!! Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuanika majina ya wasanii pamoja na askari polisi wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao wa biashara haramu ya dawa za kulevya.
Ukiachilia mbali akina Wema Sepetu, Chid Benz, TID na wengine aliowataja juzi, jana Ijumaa, Makonda alilitaja jina la Tunda pamoja na Vanesa Mdee kuwa wamo kwenye orodha ya wasanii wanatuhumiwa kujihusisha na biashara hiyo na wanatakiwa kuripoti kituoni.
Tunda
Kwa kuwa mkuu wa mkoa hakutumia majina halisi ya kuzaliwa ya wasanii hao, taarifa zilianza kusambaa mitandaoni wengine wakisema kuwa aliyetajwa ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tunda Man huku wengine wakimpigia simu kumuulizia kuhusu ukweli wa skendo hiyo.
Baada ya kuona simu zinazidi kumiminika, Tunda Man aliamua kufunguka kupitia Instagram kwamba sio yeye aliyetajwa bali aliyetajwa ndio huyo kwenye picha, akaambatanisha na picha ya Mrembo Tunda ambaye ameonekana kama video queen kwenye video nyingi za bongo fleva.
Ujumbe huo ulisomeka hivi.. “Jamani Tunda aliyetajwa na Muheshimiwa @PaulMakonda ni huyu na sio mie maana simu zimekua nyingi, @Sudibrown na wewe hujui au umeamua kunipigia tu….”