SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 6 Februari 2017

T media news

TANZIA TANZIA TANZIA


Shirikisho la Vyuo Vya Elimu ya Juu Mkoa wa Kilimanjaro kwa majonzi makubwa yasiyovumilika linasikitika kutangaza Vifo vya Wanashirikisho na wapendwa wao ambao pia ni viongozi katika shirikisho, vilivyotokea leo tarehe 05/02/2017 majira ya saa kumi na mbili jioni, huko Makelele Rombo.

Hii ni kufuatia ajali iliyohusisha, Lori aina ya Fuso, Bodaboda pamoja na gari aina ya SURF (waliyokuwa wameipanda hawa viongozi wetu). Ajali hii mbaya ilitokea baada ya Fuso hilo kukata breki na kuigonga kutokea nyuma boda boda pamoja na gari waliyokuwa wamepanda hawa viongozi wetu waliokuwa wakitokea katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika Rhombo.

Kulikuwa na jumla ya vifo vya watu 7, wanne wakiwa ni kutoka katika gari aina ya SURF lillokuwa limebeba hawa makada wa chama cha mapinduzi (CCM).

Wanashirikisho waliofikwa na mauti ni wawili yaani; *EDWIN CHRISTOPHER MSELLE* (K/Hamasa Senate Mkoa, Pia K/Mwenezi wa tawi la Tumaini KCMC) aliyekuwa *mwanafunzi wa mwaka wa nne akichukua fani ya Utabibu katika Chuo kikuu cha tiba cha KCMUCo* na *ANASTAZIA MALAMSHA* (M/kiti UWT tawi la USHIRIKA na aliyekuwa mgombea katika nafasi ya uenyekiti senate mkoa katika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi), aliyekuwa *mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha MoCU*.

Sambamba na hao, wana-CCM wengine waliofikwa na mauti ni aliyekuwa Mjumbe wa NEC *(MNEC)* kutoka Same *Bwn. Ally Mmbaga* na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana *(UVCCM)* kutoka Hai *Bwn. Anorld Swai*.

Shirikisho linawapa pole wanachama wote wa Chama cha mapinduzi (CCM) na wanashirikisho wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa msiba mzito uliowapata. Hakika hili ni pigo kwa shirikisho letu kwa kuwapoteza makada na wapambanaji waliokuwa msitari wa mbele katika kukipigania chama na Shirikisho Vyuoni.

Taratibu za Mazishi zitatolewa kadri zitakavyofahamika hapo kesho.

*MWENYEZI MUNGU ALITOA, MWENYEZI MUNGU AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. AMINA*

Imetolewa na;
*CALEB JOEL*
*_(K/Mwenezi na  Msemaji wa Shirikisho Mkoa wa Kilimanjaro)_*
+255655 884 490/+255766 884 490.