SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 4 Februari 2017

T media news

Siri Gomvi la DPP, AG Sasa Hadharani...!!


HATIMAYE siri kuhusiana na mvutano baina ya Mwansheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju na Mkurugenzu wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga,

Zimeanza kufichuka ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais John Magufuli kuwataka vigogo hao kutafuta suluhu baina yao kwa nia ya kufanikisha vyema shughuli za Serikali.

Uchunguzi uliofanywa na Nipashe kupitia vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na wawili hao na pia kwa baadhi ya wabunge wa kamati inayoshughulikia sheria na katiba, umebaini kuwa mvutano uliopo kati yao ni wa masuala mazito yanayohusiana zaidi na majukumu yao.

Chanzo kimoja cha uhakika kilisema jana kuwa mgogoro wa wawili hao ulianza kitambo na kwamba, chanzo kimojawapo kikubwa ni mamlaka aliyo nayo kikazi kila mmoja wao na pia, lipo pia suala la safari za kikazi. Juzi, akizungumza katika sherehe za Siku ya Sheria jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli aliwataka wawili hao kutafuta suluhu ya mgogoro uliopo baina yao huku akiwakumbusha kuwa wote wana nguvu kubwa kwa sababu wameteuliwa naye.