Mwaka 2016 ni mwaka ambao Shilole aliamua kuuupiga chapa kwa kufungua biashara ya mgahawa ambao ameupa jina la Shishi Food Delivery ambayo kwenye mahojiano yake kadhaa amekiri kuwa biashara hiyo inamlipa sana.
Kwenye ndoto ambazo Shilole anazo kwa mwaka 2017 na kaamua kuziweka wazi ni pamoja na kufungua kampuni (Agency) itakayokuwa inashughulika na wanamitindo wa kike na wakiume wenye ndoto za kusogea mbele zaidi upande wa fashion.
XXL ya Clouds FM ilimpata Shilole ambapo amesema>> ’Nataka kufanya kitu fulani cha modeling kwa ajili ya wasichana wapate ajira na wanaume wapate ajira,Unajua modeling sasa hivi ni biashara so watu wajiweke sawa na maumbo yao vizuri ili waweze kupata kazi toka kwa Shishi Trump baby’