SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 6 Februari 2017

T media news

Serikali yashauriwa kupiga marufuku viroba

Mbulu. Serikali imetakiwa kupiga marufuku pombe kali zinazofungwa kwenye pakiti maarufu viroba, ili kuwanusuru vijana na ulevi unaosababisha Taifa kupoteza nguvu kazi.

Mkurugenzi wa kituo cha wagonjwa wasiojiweza cha Bashay wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara, Padri James Amnaay alitoa rai hiyo juzi alipopokea msaada wa vyakula, nguo na sabuni kutoka  Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wilayani hapa.

Padri Amnaay alisema iwapo Serikali itapiga marufuku pombe hizo, itasaidia vijana kutojiingiza kwenye ulevi ambao umekithiri na kusababisha baadhi yao kuwa vichaa.

Alisema kutokana na urahisi wa kubeba na bei nafuu, pombe hizo zimewaathiri vijana wengi wanaokunywa na kulewa hatimaye kujiingiza kwenye dawa za kulevya.