SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 6 Februari 2017

T media news

MSANII ICE BOY AMBEBESHA ZIGO LA LAWAMA BARNABA

Msanii Ice Boy awali tulimtambua kama msanii wa lebo ya Barnaba Classic Boy iitwayo High Table Sound lakini siku hizi Ice boy hivi sasa anaonekana akisukuma harakati zake za mukizi yeye peke yake.

eNnewz ya EATV ikaamua kumuuliza ni kwanini ameachana na msanii mkubwa Barnaba ambaye angeweza kumsaidia kufika mbali? Katika majibu yake akaeleza kuwa alikuja kugundua kwamba huenda barnaba hakupenda yeye afanye vizuri zaidi yake na hiyo ndiyo ikawa sababu ya kuamua kufanya kazi zake mwenyewe

“Nilikuja kugundua kuwa ukimuagiza mtu front muda mwingine anaweza kukuangusha na muda mwingine siyo wote wanaopenda mafanikio lakini pia unaweza ukawa na mtu lakini hakuna lolote wengine wanakunja na hawana roho za kusaidia ndiyo maana nikaona nifanye kazi zangu mwenyewe.

Ice Boy ameendelea kusema “Kuitwa msanii wa Barnaba siyo ishu ndogo kama unavyoichukulia labda yeye anavyochukulia lakini ni ishu kama mtu unaitwa msanii wa Barnaba halafu hupigi hatua ila mimi nimetoa ngoma yangu hiyo na kila mstari nilioutoa una maana watu wanakunja sana”

Ice Boy ni moja kati ya wasanii wa Hip Hop nchini ambaye  kwa sasa anafanya vizuri na ngoma aliyomshirikisha Nandy inayoitwa Binadamu.