Kemikali iliyotumika kumuua Kim Jong Nam yagundulika
Polisi nchini Malaysia wamesema kuwa wamefichua kemikali iliyotumika kumuuwa nduguye wa kambo, kiongozi wa Korea Kaskazini, na kuitaja kuwa VX dawa ya neva. Sumu kali mno inayotumika katika vita vya kemikali. Kim Jong-nam, aliuwawa katika shambulio hilo la sumu, kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, mapema juma lililopita.Kamera za CCTV zinaonyesha wanawake wawil waliobeba vitu wakati Kim Jong nam alipokuwa akijiandaa kuingia ndani ya ndege.Korea kaskazini wiki iliyopita ilisema kuwa haitambui matokeo yeyote yatakayotokana na uchunguzi wao na kutaka warejeshewe mwili.