Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amempa siku saba ofisa elimu wa wilaya hiyo Fatma Mwiru kuhakikisha idadi ya walimu katika Shule ya Msingi Kiumbageni iliyopo Kata ya Mbweni inaongezeka.
Ametoa amri hiyo leo Jumanne asubuhi kufuatia wanafunzi wa darasa la kwanza 162 kulazimika kusoma kwenye darasa moja kwa sababu darasa lingine halina mwalimu.
Amesema haamini kama mrundikano huo wa wanafunzi katika darasa moja unatokea kwenye wilaya yake yenye walimu wa kutosha.
Amefafanua kuwa wilaya hiyo katika baadhi ya shule kuna walimu hawana cha kufanya kutokana na kuwa wengi, hivyo wapunguzwe na kupelekwa kw