Kama kuna picha umekutana nazo leo Mitandaoni zikimuonyesha Diamond Platnumz akiwa kituo cha Polisi akihojiwa nina uhakika utakua umejiuliza ni nini kilitokea.
Ni kweli leo Diamond aliitwa na Polisi na kwenye hiyo picha pia anaonekana Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Kamanda Mohamed Mpinga na kilichofanya aitwa Polisi ni ile video fupi iliyosambaa ikimuonyesha Diamond akiendesha gari bila kufunga mkanda na kucheza.
Diamond amethibitisha hilo kupitia Instagram yake kwa kuandika >> ‘picha hizo leo nilireport kituo kikuu cha polisi wa usalama barabarani kutokana na video clip tuliyopost naendesha gari barabarani bila kufunga mkanda na pia kuachia usukani na kucheza‘
‘Nikapewa Onyo na kulipa faini kwa mujibu wa sheria… tafadhali watanzania na Vijana wenzangu… tuhakikishe tunafunga mikanda pindi tupandapo na tuendeshapo Magari Maana ni Hatari kwa Maisha yetu na inaweza kukupeleka kunyea debe pia…’ – Diamond