SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 8 Februari 2017

T media news

NAY WA MITEGO ASEMA BARAKA DA PRINCE KUMSAINI LORD EYEZ NI SAFARI YA KIPOFU NA KIZIWI!

Miezi michache imepita tangu tusikie story za mkali wa kubana pua Baraka Da Prince kutaka kum-manage mkali na mkongwe wa Hiphop kutoka kampuni ya Weusi Lord Eyez.

Ikiwa ni baada ya wawili hao kukinukisha ile mbaya kwenye majukwaa kadhaa ya Fiesta msimu wa mwaka 2016.Sasa upere umefika kwa mkunaji, Nay wa Mitego amesogezewa kipaza cha Perfect255 aweze kulizungumzia suala hilo la Baraka Da Prince kumsaini Lord Eyez, jibu la Nay wa Mitego lilikuwa kama ifuatavyo.“Hiyo ni safari ya kipofu na kiziwi, naweza kusema hivyo. Kiukweli haimake sense, kwasababu mtu ambaye anataka kuongozwa na yeye akamuongoza mwenziye ndio maana ya mfano wangu. Kibaya zaidi Lord Eyez ni mkubwa zaidi ya Baraka. Sawa kuna watu ambao wanasimamiwa na watu wadogo lakini ukiangalia pale alipo msanii kama Baraka anahitaji msaada zaidi.”Hayo ni baadhi tu kati ya mengi ambayo Nay wa Mitego amefunguka juu ya mchongo huo. Bonyeza play kwenye video hii hapa chini kumsikiliza Nay akifunguka intro to outro.