SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 15 Februari 2017

T media news

Mwanamke Huyu wa Marekani Ametembelea Nchi Zote 196 na Kuweka Rekodi ya Dunia..!!


Wakati ambapo wewe hujawahi kufika katika kila mkoa hapa Tanzania, kuna mwanamke wa Marekani ambaye amefika kwenye kila nchi duniani.

Kama haitoshi, ameweza kufika katika nchi zote 196 ndani ya miezi 18 na siku 26. Cassie De Pecol amevunja rekodi ya Guinness World iliyokuwepo mwanzo.

Mwanamke huyo alianza safari yake July 2015, akipigia debe utalii endelevu kama balozi wa taasisi ya International Institute of Peace Through Tourism.

Jumla, De Pecol ametumia bajeti ya $198,000 kuizunguka dunia.