Polisi nchini Malaysia wamesema kuwa hawataruhusu kuchukuliwa kwa mwili wa kaka wa kambo wa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un hadi ambapo watapata udthibitisho kuwa watu hao ni ndugu.Mkuu wa Polisi wa Selangor, Abdul Samah Mat amesema ili waruhusu mwili wa Kim Jong Nam wanahitaji kupata ripoti ya vipimo vya DNA kutoka kwa ndugu yake wa karibu ili kuthibitisha ni ndugu yao kweli.“Bado tunasubiri maombi kutoka kwa jamaa zake, bado hatujapokea. Maombi tuliyopokea yalitoka kwa Ubalozi wa Korea Kaskazini, tunahitaji kupata DNA kutoka kwa jamaa zake ili kuwa na uhakika,” alisema Mat.Kim Jong Nam alipoteza maisha jumatatu kwa madai kuwa aliwekea sumu wakati akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kuala Lumpur alipokuwa na safari ya kuelekea mji wa Macau kwenda kuonana na familia yake.
Aidha wanawake wawili wanashikiliwa kwa kuhusika na tukio hilo, mmoja akiwa ni raia wa Indonesia na mwingine Vietnam, pia Polisi Malaysia wamemkamata mwanaume mmoja iliwasaidie kufanya upelelezi kutokana na kuwa na uhusiano na mmoja wa wanawake wanaoshikiliwa kwa madai ya kuhusika na kifo cha mtu huyo na huku wanaume wanne wakitafutwa wakihusishwa kushirikiana na wanawake hao.