Moja ya habari zilizoongozwa kusomwa kwenye mtandao wa Birminghammail, ilikuwa ni habari hii iliyowashangaza watu wengi, ambapo imeelezwa kwamba kelele za mwanadada huyo akiwa faragha zilikuwa kero kubwa kwa majirani zake.
Gemma Wale ni Mwanamke kutoka mji wa Small Heath, huko Birmigham Uingereza ambaye amejikuta akitumia adhabu ya kifungo cha wiki mbili gerezani sababu ya kuvunja sheria za kutoa sauti ya juu na kuwakera majirani zake.
Kwa mujibu wa Hakimu wa mahakama ya Halimashauri ya mji wa Birmingham, Emma Kelly amesema, Gemma Wale amevunja sheria ambayo hairuhusu watu kupiga au kutoa kelele kwa kiasi cha juu na kuwa kero kwa wengine.
Hakimu Kelly aliendelea kwa kusema, alisema sheria inakataza mtu yoyote wa mji huo kutoa au kusababisha kelele za kiwango cha juu, na kubainisha kelele kama za muziki, sherehe na vurugu kubwa. Hivyo basi baada ya kusikiliza na kufuatilia kesi hiyo kwa muda na kubainika kweli Mwanadada Wale alikuwa anasababisha kero kwa majirani zake, inabidi atumikie kifungo cha wiki mbili gerezani.
Taarifa zinazidi kueleza kwamba katika mtaa huo karibu kila jirani amelelamika kukutana na usumbufu au kero za dada huyo.
Jirani mmoja, alisema “Niliwahi kugonga mlango wake mara kadhaa na kwenda kulumbana nae kwa kelele zake, sijawahi kukutana na jirani kama huyu yani hata ukiwa mbali na upande wa pili wa barabara utasikia kelele zake pale anapokuwa faragha”.