Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla, akijibu hoja za wabunge ameviagiza vyombo vya usalama kumtafuta mtu anayejulikana kwenye mitandao ya kijamii kama "James Delicious" kwa kujitangaza kama shoga kinyume cha sheria na kumfikisha mbele ya sheria kujibu tuhuma za kuendesha biashara ya kuuza ngono ya kinyume cha maumbile.