SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 3 Februari 2017

T media news

Karibuni Katika Tanzania Business Leadership Awards Hyatt regency CHAGAMKIA FURSA 101

Tukiendelea kuchambua Fursa ndani ya filamu na muziki kuna mengi ya kushangaza katika soko hili. Fursa ya kufanikiwa katika filamu haipo Nigeria peke yake. Fursa hii inakuja kwa kasi Ghana, Afrika Mashariki na Afrika ya kusini. Najua mtaniuliza wewe Geophrey unayajuaje hayo? Nafanya utafiti. Idadi ya watu Afrika hasa Afrika Mashariki inakua kwa kasi sana. Hii ni fursa kubwa kwa watu wajanja watakaoandaa bidhaa zinazohitajika kwa watu hawa. Kulingana na utafiti uliofanywa na BBC, walaji na watumiaji  wakubwa wa filamu wapo Afrika. Na ili uweze kutengeneza filamu ya viwango inaweza kukugharimu $25,000 mpaka$50,000 sawa sawa na TZS 50millioni mpaka millioni 100 TZS.

Na filamu hiyo inaweza kutengenezwa kwa muda wa mwezi mmoja mpaka miwili. Najua kuna watu watashtuka hapa. Ukiweza kutengeneza filamu hiyo kwa kulenga soko lote la Afrika- ndani ya wiki mbili tatu, kulingana na utafiti wa BBC unaweza kutengeneza faida mara mbili ya gharama uliyotumia. Na ukiwa mjanja unaweza kuendelea kula faida ya filamu hiyo moja mpaka kizazi cha pili cha tatu na kuendelea. Kilichokosekana katika filamu, kwanza ni wajasiriamali wajanja. Wengi wetu tunadanganywa na fursa zisizo na kichwa wala mkia.
Unakumbuka fursa ya mayai  ya kware? Iko wapi sasa?
Tulisikia wote kelele na ngonjela kuwa mayai ya kware ni dawa- niambie kilichotokea? Watu walitupa pesa zao kama vichaa. Yako wapi mayai ya kware Leo?

Narudia tena kufanikiwa kibiashara Africa huitaji mikwara mingi kiivyo. Jifunze kutofautisha kipi ni kipi . Leo hii kuna Kampeni ya sungura, Labda kesho itakuja Kampeni ya Nkoma... Sijui.

Nifuatilie Katika fursa 101 kila sekta itaguswa huitaji kupelekeshwa kwa Kampeni.

Karibuni Katika Tanzania Business Leadership Awards Hyatt regency

0655 973 248