SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 6 Februari 2017

T media news

JOSLIN ATAJA SABABU ZA KUNDI LA WAKALI KWANZA KUSHINDWA KURUDI KWENYE MUZIKI


 

Msanii wa bongo fleva Joslin kutoka kundi la 'Wakali Kwanza', ameeleza sababu ya kundi hilo kushindwa kurudi kwenye game, licha ya kuahidi mashabiki kuwa mwaka 2016 wangerudi kwa moto ule ule wa enzi zile.

Kipindi cha eNewz cha EATV kilizungumza na Josline baada ya kuona kimya kimezidi na kutaka kujua ni nini kilichowakwamisha wasanii hao tangu mwaka 2016 walipoweka wazi kuwa wanarudi tena ambapo amesema kinachowakwamisha ni kukosa ushirikiano kutoka kwa watu fulani fulani ambao hakuwaweka wazi huku akitamba kuwa wao kama wakali kwanza huwa wanafanya vitu vya kudumu

“Unajua sisi huwa tunafanya vitu ambavyo ni vya kudumu sana na watu tofauti na wasanii wengine huwa tukifanya ngoma nyimbo zetu zinakaa kwa muda mrefu sana ukiangalia mimi Josilin na Wakali kwanza hata ukiingia sehemu unakuta mtu anakuita, angalia ngoma kama Niite basi, Perfume na unakuta unaangalia muda mwingine tunakosa support kwa watu wawili watatu na sasa hivi imekuwa kama ni story ya uongo tu”

Wakali kwanza ni moja kati ya kundi la wasanii ambao waliwahi kufanya vizuri katika game ya bongo fleva miaka miaka ya nyuma lakini kwa sasa bado hawajaweza kurudi tena kwenye game.

Kundi hilo lilikuwa linaundwa na wasanii watatu ambao ni Makamua, ,Josilin pamoja na Qj .