Mchezaji wa zamani wa Chelsea na Kiungo wa Timu ya Taifa ya Uingereza Frank Lampard ametangaza rasmi kutandika Daluga na kusalia kuwa mtazamaji na kuchukua mafunzo ya Ukocha.
Frank Lampard amenyakua mataji matatu ya EPL,Makombe manne ya FA,vikombe viwili vya kombe la Ligi,Taji moja la Klabu Bingwa Ulaya na Europa,na kumfanya atimize michezo 1039 na Magoli 302 kwa miaka 21 aliyoitumikia kama mchezaji kwenye vilabu mbalimbali na Timu yake ya Taifa.