Singida. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba amesema watu wanane wameshambuliwa na fisi kati ya Februari 14 na 16.
Kutokana na hali hiyo, jana Magiligimba ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari na kutoa taarifa mapema pindi wawaonapo wanyama hao ili wadhibitiwe.
Amesema kuna baadhi ya familia zinazoishi kwenye nyumba maarufu tembe huweka milango imara ili kuwadhibiti fisi hao wasiingie ndani kirahisi.
Kamanda huyo ametoa wito pia kwa wanafunzi waendapo shuleni na wanaporejea jioni kuchukua tahadhari.
Amesema Februali 14, Ofisa Mendaji wa Mgongo, Mwajuma Lugamba (42)l alishambuliwa na fisi alipokuwa akirejea nyumbani akitokea kazini.
Amesema siku hiyo hiyo, watu wengine Masunga Ngusa (47) na Nkhamba Ngusa (27), walivamiwa na fisi walipokuwa wamelala kwenye nyumba yao ya tembe.
Wengine waliojeruhiwa ni Sunday Msengi (21) Faidda Ramadhan (9), Charles Juma (45),Yusuph Ally (22) na Ramadhan Juma (60)