SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 14 Februari 2017

T media news

Familia ya Sadio Mane yavamiwa


Bado Wasenagal wanaumizwa sana na tukio la timu yao kuondolewa katika mashindano ya Afcon.Raia wengi wa Senegal pamoja na mashabiki wengi wa soka waliamini kwamba Senegal wanaweza kuchukua ubingwa wa Afcon.Alikuwa ni mchezaji wao tegemezi Sadio Mane ambae alikosa tuta lililowapelekea Senegal kuondolewa katika mashindano hayo.

Sasa familia ya Sadio Mane iliyoko huko Senegal imekumbana na majanga ambayk yamesababishwa na kukosa penati kwa Mane.Familia ya mjomba wake Mane imevamiwa na kikundi cha wahuni ambao inasemekana walikuwa na nia ya kumdhuru mjomba wake huyo.

Mjomba wake Mane na wanafamilia yake wameripoti tukio hilo Katika tukio hilo vibaka hao waliharibu gari ya mjomba yake Mane ambayo alinunuliwa na Sadio Mane kwa kiasi cha £ 24,000.Watu walioshuhudia tukio hilo walisema kikundi hicho kilivamia kwa hasira familia ya wakina Mane na kuanza kulupiga piga gari hilo lililokuwa nje ya nyumba yao huko Malika.

Wakati familia yake ikitokewa na majanga hayo Mane yeye alikuwa busy na Liverpool.Mane alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu akiiongoza timu yake kuifunga Tottenham magoli mawili kwa sifuri huku kocha wake Jurgen Klopp akimmwagia sifa kwa kusema hakuna timu yoyote ambayo isingeathirika kumkosa Sadio Mane.