Msanii wa muziki na baba wa mtoto mmoja, Rich Mavoko amedai katika maisha yake ya muziki haoni sababu ya kumwanika mpenzi wake katika mitandao ya kijamii.
Muimbaji huyo wa WCB ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kokoro’ aliyomshirikisha Diamond, amedai yeye siyo mtu wa kutangaza masuala ya mahusiano yake kwenye mitandao kama wasanii wengine.
“Nina mpenzi pamoja na mtoto lakini sipendi tu kuwaanika mitandaoni,” alisema Rich Mavoko. “Labda muda bado siwezi kusema kwamba sitampost mpenzi wangu Instagram katika maisha yangu yote lakini mashabiki wangu wanajua Richard ni mtu wa aina gani, kwahiyo tuache waendelee kumwangalia Rich Mavoko kwa jicho hilo,”
Alisema kila msanii ana namna ambavyo anaweza kuchanganya masuala ya mahusiano yake na muziki lakini yeye hawezi kufanya hivyo kwa kuwa kila kitu kinajitegemea.
Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili kazi mpya ambazo zitakuwa pamoja na kolabo mpya za kimataifa.