Zari the Bosslady amekiri kuwa uraia wa mwanae wa kiume, Nillan uko ‘complicated’ kidogo.
Kwenye mahojiano yake na Dizzim Online, mchumba huyo wa Diamond amesema pindi tu mtoto wake amezaliwa huko nchini Afrika Kusini, alipewa uraia wa nchi hiyo.
“Yaani hiyo iki complicated because amezaliwa kule akapata immediate citizenship lakini vile amerudi nyumbani sasa hivi tutarudisha ile citizenship ya South Africa halafu atachukua ya Tanzania,” alisema Zari.
40 ya Nillan ilifanyika Jumamosi iliyopita nyumba kwa Diamond, Madale jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao. Ni mtoto wao wa pili baada ya Tiffah mwenye mwaka mmoja na miezi kadhaa sasa. Tiffah alizaliwa Tanzania.