SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 18 Februari 2017

T media news

Duh..Noma Sana ...Kocha Afukuzwa kwa Kukataa Kuroga..!!!


KOCHA wa timu ya Mzimuni FC ya Sarawak mkoani Pwani, Ally Yusuf ‘Ostadh’, hivi karibuni alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutimuliwa kikosini kisa kikitajwa ni kukataa kukubali kuroga kabla ya mechi.

Ostadh ambaye alikuwa akikiandaa kikosi chake kukabiliana na Sunderland FC kwenye michuano ya Kombe la Jezi, alipotakiwa na uongozi wa timu hiyo kukubali kuroga ili washinde kirahisi, alikataa kwa kusema imani yake ya dini haimruhusu kufanya hivyo.

Ostadh alisema: “Unajua tangu mwanzo tulikuwa tukishinda bila hata ya kufanya hivyo, lakini baada ya kuona tumefika hatua ya nusu fainali halafu tunakutana na timu ngumu, wakasema tukaroge, nikakataa kwa sababu dini yangu hairuhusu mambo hayo, wakanitimua, lakini kichapo walichokutana nacho cha mabao 3-0 kimekuwa fundisho kwao.”