SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 3 Februari 2017

T media news

BARUA kwa Rais na Watanzania wote YAH: FURSA 101 ZA KIBIASHARA AFRIKA!



Mhe. Rais pamoja na Watanzania wenzangu.

Wengi wetu tunaamini kuwa ili uweze kuanzisha na kufanikiwa kibiashara unahitaji mambo makuu mawili:
1. Wazo bunifu na kubwa la biashara.
2. Mtaji mkubwa na wa kutosha kuanzisha biashara.

Ukweli ni kuwa siyo lazima uwe na hayo yote. Afrika ni tofauti. Ili ufanikiwe kibiashara Afrika siyo lazima ufanyiwe miujiza. Inahitaji akili ya kawaida sana. Unaona? Ni rahisi Afrika.

Afrika inahitaji wafanyabiashara wa kawaida wanaoweza kutoa huduma na bidhaa zinazohitajika kila siku.

Afrika ni soko linalokua kwa kasi sana zaidi ya kawaida. Afrika inahitaji kila kitu. Afrika bado ni mbichi kibiashara. Wengi waliofanikiwa kibiashara Afrika kama akina Aliko Dangote, Bakhresa, Mohamed Dewji, Strive Masiyiwa na wengine wengi ni watu wa kawaida sana hawakuja na mawazo makubwa sanaa. Walianza kutoa huduma na kuuza bidhaa za kawaida zinazohitajika Afrika kila siku na wakatajirika.

Wapo wengine walioanza na mtaji mdogo sana lakini leo hii wanaendesha biashara kubwa AFRIKA.
Ili ufanikiwe kibiashara Afrika usisukumwe na malengo ya kupata pesa nyingi kwa mwanzo. Hakikisha unasukumwa na malengo ya kuifanya Afrika iwe ya tofauti. Afrika ipanuke. Afrika ibadilike. Afrika Ikue. Fikiria ni vipi utawafanya waafrika wenzako wafurahie, wafaidike na wabadilishwe na huduma au bidhaa zako. Ukianza hivyo pesa zitakuja kwako kwa kasi sana. Kizazi cha Afrika kinahitaji waafrika makini, chanya na waliotayari kuibadili Afrika.

Hebu fikiria Marekani-mtoto akizaliwa anafundishwa na kuaminishwa jinsi ya kuhudumia dunia nzima

Mtoto akizaliwa Africa-Manzese anafundishwa jinsi ya kuuza karanga manzese mtaa wa Pili.

Unadhani kwanini maduka Mengi yamefungwa kwasasa?

Ni kwasababu akili zetu zimejengwa ku-operate locally. Tutamlaumu Magufuli bure.
Fikiria Kama ungekuwa na biashara mbili tatu Katika nchi tatu ingekuwaje?

Ni rahisi Sana kufanya biashara Africa.

Afrika ni taifa rahisi kufanikiwa kibiashara. Najua wengine tunalalamika RUSHWA AFRIKA, UONGOZI MBAYA AFRIKA, MAZINGIRA WEZESHI MABOVU, UGAIDI, USALAMA MBOVU AFRIKA. Hayo yote yasikukukatishe tamaa na kukufanya ubaki chini kimaisha. Ni kweli matatizo ni mengi Afrika lakini siyo sababu ya wewe kushindwa kusimamisha na kufanikiwa kibiashara. Zipo kila sababu kwanini ni rahisi kufanikiwa kibiashara AFRIKA kuliko sehemu yoyote duniani.
Hapa pichani bw fursa 101 kiongea na wadawa walio fanikiwa.



Nina marafiki Wengi US, Ukraine,  India wanaokimbilia Africa na kufanikiwa.

Africa ina nchi 54 kila nchi ina tabia yake, sheria zake na mipango yake ya kupambana na Rushwa na Fursa zake. Ili ufike mbali kimataifa lazima ujue FURSA zote zilizopo AFRIKA siyo manzese peke yake. Panuka Ndugu yangu.

 Hakikisha unaijua AFRIKA kuliko hata mtaa wako uliozaliwa au kukulia.
Hebu tuweke pembeni sababu za kwanini huwezi kufanikiwa kibiashara Afrika na tuamue sasa kutafuta sababu za kwanini ni rahisi kuanzisha na kufanikiwa kibiashara Afrika kuliko nchi yoyote Duniani.

“Binadamu aliye kwenye hatari si yule aliyechukua maamuzi yanayoogopesha na kutisha bali ni yule anayeogopa kuchukua maamuzi hayo kwasababu anaogopa”

Uchumi wa Afrika unaendelea kukua na kukua. AFRIKA imejaa FURSA nyingi zisizohesabika.
Najua biashara si kwaajili ya kila mtu, haitakiwi kuwa hivyo. Lakini kama ni mmoja wa wale watu wachache wenye moyo wa kutaka kufanya kitu cha tofauti, wenye malengo ya kusimamisha biashara zao kubwa AFRIKA huu ni wakati wako.

Fursa zipo  Afrika!!

Upo tayari kwaajili ya AFRIKA?
Amini usiamini AFRIKA ipo tayari kwaajili yako.
Kabla hatujaanza kuchambua FURSA 101 za kufanikiwa kibiashara AFRIKA naomba nikukumbushe jambo muhimu hapa: Hakikisha unafuatilia kwa makini kila fursa, zielewe, fahamu masoko yake, changamoto zake na chagua FURSA chache unazoamini zitabadili maisha yako kisha chukua hatua. Narudia tena chukua hatua.
Ninaamini kuwa mawazo na FURSA utakazogundua kuanzia sasa utazifanyia kazi kwasababu utaonyeshwa njia jinsi ya kufanya, wapi upite na wapi uende.
FURSA zilizochambuliwa humu ndani hazihitaji mtaji mkubwa lakini zinahitaji nguvu kubwa ya utayari na kujituma, nidhamu na uvumilivu.
FURSA 101 hazihitaji wewe uwe na akili sana katika kile utakachochagua kufanya. Unaweza kuwa bora AFRIKA nzima katika FURSA utakayochagua hata kama hukusomea .

A: FURSA KATIKA BURUDANI.
“Hatupo katika kizazi cha taarifa na maarifa. Tupo katika kizazi cha BURUDANI na STAREHE .” Tony Robbins

Burudani ni biashara inayokuwa kwa kasi sana AFRIKA zaidi ya kawaida. Sekta ya burudani imejaa fursa nyingi sana kwa wajasiriamali makini.
Kila siku mamilioni ya watu duniani wanahangaika kutafuta sehemu za kustarehe, vitu vya kujistarehesha na kujiburudisha, michezo na matamasha ya kufurahisha.
Burudani ni sekta inayokua kwa kasi sana Afrika zaidi ya kawaida. Yeyote atakayeamua kuichunguza sekta hii atashangaa fursa zilizojaa.
Sekta ya burudani inatengeneza zaidi ya $50 billioni kila mwaka. Sekta hii inaongoza katika kutengeneza ajira kuliko sekta zote Afrika.
Afrika ikiwa kama sehemu ya kivutio cha utalii, vipaji vya filamu na muziki bado vibichi. Dunia nzima inahamia Afrika kwasababu Afrika inaendelea kukua na kukua katika sekta ya burudani. Wengi wetu bado hatujatumika. Bado wabichi. Hapa nilipo nina zaidi ya vitabu kumi ambavyo vinavyoweza kutengenezwa filamu za kimataifa na kimapinduzi. Si mimi peke yangu nimekutana na vijana wenye vipaji vya kutisha. Sikiliza vijana katika redio na televisheni mbalimbali Afrika utagundua mengi ya kushangaza.
Katika sekta hii tutagusia sehemu chache sana...tano tu. Nikiamua kuandika kitabu kuelezea fursa zilizopo katika sekta hii ni zaidi ya vitabu viwili. Ngoja nikupe dondoo chache kuhusu Fursa katika burudani.

1. FURSA KATIKA FILAMU NA MUZIKI.
Filamu na muziki! Mungu wangu!!!!!! Sijui nianzie wapi hapa. Sekta ya Filamu na muziki inakuja kwa kasi zaidi ya kawaida. Imejaa vipaji visivyo na kikomo. Hii fursa bado mbichi sana. Angekuwa mwanamke ningesema hii fursa ni bikra. Bado haijaguswa vya kutosha. Kila siku makampuni ya filamu, sanaa na habari yanasajiliwa kila siku. Mwaka 2015 GDP yake imekua kwa 5%. Ukichunguza waigizaji, waimbaji kama akina Diamond Platnum wanaingiza pesa nyingi kwa mwezi kuliko wakurugenzi wakubwa Afrika. Hata ukiwa fisadi serikalini huwezi kushindana nao. Sekta hii Imejaa pesa nje nje kuliko kawaida. Laiti kama Merehemu Kanumba angekuwepo tungekuwa tunaongea lugha nyingine katika sekta ya filamu. Nimekutana na waigizaji wengi kama akina Gabo na wengine wengi maarufu…nasikitika kusema kuwa bado hawajagusa hii sekta.
Wako wapi wafanyabiashara wajanja afrika waweze kuichangamkia sekta hii jamani?
Tukianza na Nollywood, huko Nigeria. Unapoongelea Nollywood wamegusa kiasi kidogo sana katika sekta hii ya filamu Afrika. Yaani bado. Nollywood tu peke yake ina thamani ya $800 millioni. Katika nchi kama Nigeria yenye matatizo ya ukosefu wa ajira, Nollywood peke yake inaajiri zaidi ya mamilioni ya watu na kuifanya sekta hii ya filamu kuongoza baada ya sekta ya kilimo. Wapo wasomi wengi mitaani wamefungwa na vyeti vyao wana vipaji na hata uwezo wa kuanzisha makampuni ya filamu Tanzania lakini wamelala fofo. Usingizi mzito..
Nimekutana na vijana wa kawaida sana hawajaenda hata shule, hawajui hata kuandika lakini katika sekta hii...wamejiajiri wanaingiza pesa za kutosha kila mwezi kuliko hata mameneja wa Benki. Wanamiliki makampuni tena mengine hayajasajiliwa. Endelea kung’ang’ania cheti...tuone kitakufikisha wapi.
Waafrika wengi wanapenda starehe. Narudia tena...waafrika wengi wanapenda kuburudishwa. Hii ni fursa. Tangu Nollywood ianzishwe imekua kwa kasi sana sana.... na kuchukua nafasi ya pili duniani baada ya Bollywood katika idadi ya filamu zinazotengenezwa kila siku. Nollywood inatengeneza filamu 2000 kila mwaka baada ya Bollywood kutoka india inayotengeneza filamu 3000 kwa mwaka. Ikifuatia na Hollywood , Marekani inayotengeneza filamu 800 kwa mwaka.
Fursa katika filamu na muziki ni zaidi ya kawaida hapa Afrika. Waulize akina Joseph Kussaga mmiliki wa Clouds Media Group utashangaa pesa anazoingiza…mpaka kufungua makampuni mengine zaidi Dubai. Waulize Steps Entertainment na wengine wengi utashangaa. Wewe endelea kushangaa wakati wenzako wanatengeneza pesa.
Idadi ya watu Afrika inakua kwa kasi sana. Matatizo ya usambazaji wa kazi za sanaa, muziki na filamu inaifanya Afrika kuwa mbichi sana katika sekta hii. Sasa kwa watu wenye mawazo hasi wataishia kuongelea matatizo yaliyopo ndani ya sekta hii. Nikuambie ukweli yeyote atakayeingia na kutatua matatizo yaliyo ndani ya sekta hii ni billionea wa Afrika. Waulize akina Wema Sepetu, Erick Shigongo, Ruge Mutahaba, Paul Mashauri na wasanii wengine wengi Tanzania wana filamu ngapi zilizochezwa lakini wameziweka kapuni kwasababu hajatokea mjasiriamali mjanja Afrika anayeweza kutatua matatizo yaliyo ndani ya Sekta hii upande wa usambazaji.
Milango iliyofunguliwa na Fursa hii: Fursa hii imefungua milango mingine zaidi ya fursa nyingine. Wanatafutwa watu na makampuni katika utengenezaji wa filamu na muziki. Wapiga picha makini hakuna Tanzania. Editors wa filamu bado...akina Diamond Platnum wanakimbilia Afrika kusini kwasababu bado hawajatokea watu makini wa kuishika vizuri sekta hii. Watalaamu katika animations, Mavazi na mapambo kwaajili ya filamu bado. Watengenezaji wa sauti na zaidi. Hizo zote ni fursa ambazo hazijaguswa. Nyie endeleeni kuuza vibanda na maduka ya vocha wakati kuna wajanja wanatengeneza mamilioni ya pesa katika filamu.
Ernest Napoleon alipokuja Tanzania kwaajili ya kuandaa waandaaji wa filamu yake mpya iitwayo GOING BONGO alihangaika sana kupata waandaaji Tanzania. Yaani alichoka mwenyewe, ikabidi aende Kenya na kurudi Marekani kutafuta watu wengine makini.
Filamu zinazotengenezwa kila siku Tanzania ni za viwango vya chini. Yaani ni vichekesho. Akitokea mfanyabiashara makini akafanya kitalaamu na kuwaongoza vijana waigizaji na waimbaji hapa Tanzania, ni Tajiri. Muulize Mkubwa na wanae anavyotamba.
Katika usambazaji ndiyo basi kabisa. Hii ni fursa kubwa zaidi ya maelezo. Ni nani anayeweza kutatua matatizo ya usambazaji wa kazi za sanaa? Ukitafuta njia za kusambaza kazi za sanaa kifaida kama mjasiriamali, wasanii wote watakukimbilia wewe.

Muulize Nadeem Juma wa Mkito akuambie pesa anazoingiza.

Upande wa tamthilia bado kabisa. Vipindi vya televisheni vinavyoonyesha maisha halisi bado hata kidogo. Sijaona. Ukikaa kuanzia asubuhi kuangalia televisheni za Tanzania utachoka mwenyewe. Utajikuta unasinzia. Hakuna vipindi. Narudia tena hakuna vipindi vinavyogusa. Umewahi kukiona kipindi Tanzania katika televisheni ukatamani ununue hicho kipindi uwe unaangalia kila siku nyumbani? Hakuna. Bado fursa hii ni mbichi. Vipindi vyenyewe vinavyoandaliwa bado havionyeshi umakini. Ni nani mjasiriamali anataka kuichangamkia fursa hii jamani? Mko wapi mtuokoe katika burudani ili tufurahie kuishi duniani jamani?
Nani Amefanikiwa katika sekta ya filamu!
Katika Tanzania tunawajua wengi waliopiga hatua katika burudani. Kabla sijakutajia majina ya watu waliofanikiwa katika sekta hii ngoja nikupe stori fupi ya Jason Njoku wa iROKOtv(Nigeria)

Mwaka 2010, Jason Njoku akiwa anaishi Uingereza na mama yake, aliombwa na mama yake amtafutie filamu nzuri ya kinigeria kupitia mtandao. Alihangaika weee lakini hakuweza kupata filamu. Akagundua kuwa filamu nyingi Afrika zinasambazwa kwa njia ya kikawaida sana kupitia DVD. Kwanza njia hii ni rahisi kuibiwa kazi.
Akajiuliza sasa watu walio nje ya Afrika au mbali na Nigeria wakitaka kuona filamu kirahisi watafanyaje? Akagundua fursa. Akaamua kurudi kwao Nigeria na kwenda kuomba kibali cha usambazaji wa filamu kwa njia ya mtandao. Akakubaliwa. Leo hii anasambaza filamu kwa njia ya mtandao, zipo zaidi ya filamu 5000 ndani ya mfumo wa mtandao kupitia iROKOtv.
Gazeti la forbes wameitaja iROKOtv kama Netflix ya Afrika. iROKOtv inatembelewa na zaidi ya watu millioni 10 kwa mwezi. Amekusanya zaidi ya $12 millioni kutoka kwa wawekezaji. Kila mwezi anaingiza zaidi ya $1 millioni.
Leo hii Jason amefungua tena mtandao mwingine uitwao iROKING.....kama mtandao wa kusambaza miziki ya wasanii Afrika. Jason ni millionea wa Afrika. Alichukua hatua baada ya kugundua matatizo ya usambazaji wa kazi za sanaa. Naomba nikukumbushe kuwa wakati unalalamika..sijui Magufuli amebana pesa…sijui Magufuli ameziba hiki na kile…wenzako wanagundua matatizo na kutengeneza pesa kupitia matatizo.
Sikiliza nikuambie kitu...kipindi kama hiki ambacho Tanzania inapitia Hali ngumu kitaamsha watu wenye akili na wajanja na kutupa kule wale wote waliofanikiwa kwa mteremko na Njia rahisi rahisi. Achana na wanasiasa wanakupigia kelele ili kujenga nguvu zao kisiasa.

Ukitaka kujua zaidi kuhusu fursa hizi Nifuatilie... Na utaunganishwa whatsapp kwa 0655973248.

Geophrey Tenganamba
CEO GCP