MSANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha amefunguka kuwa licha ya mastaa wengi kuwa na wasiwasi wa kutajwa majina yao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kama wengine, yeye hana shaka kwani hatumii na wala hana marafiki wanaojihusisha na ishu hiyo.
Baby Madaha
Baby Madaha
Akipiga stori na Risasi Vibes, Baby Madaha alisema hana wasiwasi wa kuitwa kwa sababu hajawahi kutumia na hana kampani ya wanaotumia kwa sababu akianza urafiki na mtu huwa anamfanyia uchunguzi kwanza na akiona haelekei, anampotezea.
“Sijawahi kutumia unga wala sina kampani ya wanaotumia au kusafirisha, maana marafiki zangu wote na watu wa karibu kabla sijaanza ukaribu nao huwa nawachunguza kwanza, hivyo najiamini na Watanzania wanatakiwa watambue kuwa Makonda hajakurupuka, vita ndiyo imeanza na mifano hai itatokea kwetu sisi wasanii,” alisema Baby Madaha.